MARUDIO YA KCSE: KISWAHILI KARATASI YA TATU, 102/3_ UCHAMBUZI WA  TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE

Jinsi ya kujibu maswali ya Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine

Utangulizi

 • Diwani Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine ina hadithi 13.
 • Hadithi hizi ni zifuatazo:
 1. Tumbo Lisiloshiba
 2. Mapenzi ya Kifauroongo
 3. Shogake Dada ana Ndevu
 4. Shibe Inatumaliza
 5. Mame Bakari
 6. Masharti ya Kisasa
 7. Ndoto ya Mashaka
 8. Kidege
 9. Nizikeni Papa Hapa
 10. Tulipokutana Tena
 11. Mwalimu Mstaafu
 12. Mtihani wa Maisha
 13. Mkubwa

Maswali ya Diwani

 • Maswali katika Diwani huwa ni ya aina mbili:
 1. Maswali ya dondoo
 2. Maswali ya Insha

 

 1. Maswali ya Dondoo
 • Ni maswali yanayojikita katika muktadha fulani
 • Katika kujibu maswali ya aina hii, mtahiniwa anatarajiwa kuchukua mkondo wa kawaida unaochukuliwa katika kujibu maswali ya dondoo.
 • Anapaswa kutaja msemaji, msemewa, sababu ya maneno yale kusemwa na ni wapi yanaposemwa ili kupata alama nne (4) zinazotengewa swali la sampuli hii.
 • Basi vipengele vifuatavyo huzingatiwa:
 1. Msemaji
 2. Msemewa
 3. Mahali /Eneo/Mazingira alipo msemaji
 4. Sababu ya kusema maneno hayo
 • Swali la aina hii hufungamanishwa na maswali ya mbinu za lugha pamoja na ya maudhui.

 

Kwa mfano:

SEHEMU YA A: HADITHI FUPI (alama 20)

Kenna Wasike: Mapenzi ya Kifaurongo

“Na nyumba hii uione paa. Nipite juu upite chini.”

 1. a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
 2. b) Bainisha mbinu nne za lugha zionazojitokeza katika dondoo hili. (alama 8)
 3. c) Kwa kurejelea hadithi nzima, thibitisha kuwa asasi ya elimu inakabiliwa na changamoto chungu nzima. (alama 12)

Mwongozo

 1. Ni maneno ya Penina

Anamwambia Dennis

Walikuwa chumbani mwa Penina

Penina alisema haya baada ya Dennis kurudi nyumbani na kumwambia kuwa hajafanikiwa kupata kazi.

 1. Jazanda-uione paa kuashiria asirudi huko tena

Nahau -ona paa

Litifati-“Nyumba hii uione paa “

Taswira-paa

 1. Umaskini

Ubaguzi

Mapuuza

Ukosefu wa walimu

Ukosefu wa madarasa

Mapenzi y’all kiholela

Utabaka

Mimba za mapema

Tanbihi: Hoja zitajwe na kutolewa ithibati kwa kurejelea wahusika mbalimbali katika hadithi.

Mfano : Mimba za mapema. Safia anapata ujauzito akiwa mtoto mdogo na kuamua baadaye anaaga dunia anapotaka kuavya mimba hiyo.

 1. b) Maswali ya Insha
  • Maswali ya aina hii hurejelea hadithi zaidi ya moja.
  • Mtahiniwa anatarajiwa awe amesoma na kufasiri hadithi zote 13 ili kujibu swali kama hili kwa wepesi na ufasaha.
  • Kuna uwezekano wa mtahiniwa kuelekezwa kwa kupewa hadithi za kurejelea au huenda akapewa nafasi kuchagua hadithi zozote zilizo na suala lililoulizwa (hili huwa nadra).
  • Katika swali hili, mtahiniwa anatarajiwa kufungamanisha hoja zozote atoazo na mhusika (kutoa ithibati au kuthibitisha) ili aweze kupata alama.
  • Swali hili huweza kutahini maudhui, mbinu mbalimbali za lugha au hata wahusika mbalimbali.

Kwa mfano:

SEHEMU YA A: HADITHI FUPI (alama 20)

 1. Ndoa inakabiliwa na changamoto nyingi sana katika diwani Tumbo lisiloshiba. Thibitisha kwa kurejelea hadithi zifuatazo:
 2. a) Mtihani wa maisha
 3. b) Shogake Dada ana Ndevu
 4. c) Masharti ya Kisasa
 5. d) Mwalimu Mstaafu (alama 20)

Hoja za kuzingatiwa

 1. Mtihani wa Maisha
 • Utamaushi
 • Migogoro ya kifamilia
 • Ubaguzi wa kijinsia
 • Udanganyifu
 • Kudharauliwa kwa mtoto wa kike.
 1. Shogake Dada ana Ndevu
 • Mimba za mapema.
 • Utepetevu katika malezi
 • Uavyaji mimba
 • Mapenzi ya kiholela.
 • Udanganyifu
 • Mauti /kifo.

 

 1. c) Masharti ya Kisasa
 • Migogoro ya kifamilia.
 • Ukosefu wa maarifa/elimu.
 • Kutoaminika katika ndoa.
 • Kazi duni.
 • Wanawake kufanya kazi za usiku.
 • Wanawake kutotaka kushiriki majukumu ya nyumbani kikamilifu.
 1. Mwalimu Mustaafu
 • Ulevi
 • Umaskini
 • Ukosefu wa ajira.
 • Unyanyasaji/dhuluma kwa wa kike.
 • Utepetevu katika malezi ya watoto.
 • Ubabedume/Taasubi ya kiume.

Tanbihi: Katika hoja zote jadili kikamilifu kwa kuthibitisha kutumia wahusika mbalimbali ili kupata alama.

 1. Linganisha na ulinganue wahusika Mzee mambo katika hadithi shibe inatumaliza na Mkubwa katika hadithi Mkubwa. (alama 10)

AU

 1. Jadili jinsi mwandishi alivyotumia mbinu ya uzungumzi nafsi kufanikisha ujumbe katika hadithi Mame bakari na Mtihani wa Maisha. (alama 20)

Kielelezo

 • Katika maswali kama hayo yaliyopewa juu, mtahiniwa huhitajika kuchagua swali moja na kulijibu kwa ufasaha.
 • Mtahiniwa achague swali analolitambua vyema na ambalo ataweza kutoa hoja kadri mtahini anavyohitaji kikamilifu.
 • Epuka swali ambalo huna hoja za kutosha.
 • Katika swali la kulinganisha na kulinganua; Anza kwa kutoa mfanano uliopo kati ya wahusika uliopewa kisha fafanua tofauti kati yao vilevile bila kuchanganya.
 • Swali la mbinu lijibiwe kwa kutoa mifano mwafaka kutoka hadithi zilizopeanwa.

Maelezo ya jumla

 • Kuna maudhui ya jumla yanayojitokeza katika hadithi zaidi ya nne kwenye Diwani.
 • .Maudhui haya ni kama vile;
 1. Ndoa na changamoto zake
 2. Malezi na changamoto zake
 3. Elimu, umuhimu wake na changamoto zake.
 4. Umaskini.
 5. Ukatili.
 6. Mapenzi.
 7. Unafiki/uongo
 8. Nafasi ya vijana katika jamii.
 9. Nafasi ya wanawake katika jamii.
 10. Tamaa.
 11. Ubadhirifu/ufisadi
 12. Usaliti
 13. Mapuuza/ujinga
 14. ubinafsi

Maswali ya kutarajiwa

 • Haya ni makadirio/makisio tu ya sehemu za kutahiniwa katika kila hadithi.
 • Haya ni kama yafuatayo;
 1. 1. Tumbo Lisiloshiba
 • Maudhui ya ukatili /ubinafsi
 • Mbinu ya jazanda
 1. Mapenzi ya Kifaurongo
 • Maudhuo ya umaskini/elimu na changamoto zake/utabaka
 1. Shogake Dada ana Ndevu
 • Maudhui ya malezi na changamoto zake/mapuuza na madhara yake.
 1. Shibe Inatumaliza
 • Maudhui ya ufisadi/ubinafsi/ubadhirifu
 • Mbinu ya taswira
 1. Mame Bakari
 • Maudhui ya ukatili/nafasi ya mwanamke katika jamii
 • Mbinu za uzungumzinafsi na kisengerenyuma
 1. Masharti ya Kisasa
 • Maudhui ya ndoa na changamoto zake/ ukengeushi-usasaleo
 1. Ndoto ya Mashaka
 • Maudhui ya umaskini/ndoa na changamoto zake/ubaguzi/utabaka
 • Mbinu ya jazanda
 1. Kidege
 • Maudhui ya utawala mbaya /unyanyasaji /matumizi mabaya ya mamlaka na rasilimali
 • Mbinu za jazanda na taswira.
 1. Nizikeni Papa Hapa
 • Maudhui ya usaliti/kutowajibika
 1. Tulipokutana Tena
 • Maudhui ya Ukatili/Ushirikina
 • Mbinu za sadfa na taswira
 1. Mwalimu Mstaafu
 • Maudhui ya Elimu, umuhimu na changamoto zinazoikumba/malezi
 • Mbinu ya kinaya
 1. Mtihani wa Maisha
 • Maudhui ya Elimu/malezi
 • Mbinu za uzungumzi nafsi na kinaya
 1. Mkubwa
 • Maudhui ya utawala mbaya/matumizi na ulanguzi wa mihadarati/athari za mihadarati

 TANBIHI:

Mtahiniwa aangazie kila sehemu kwa jumla bila kupuuza chochote. Yaliyoangaziwa ni mwelekeo na utaratibu tu wa jinsi ya kushughulikia maswali ya hadithi mbalimbali katika diwani na baadhi ya maswali yanayotarajiwa kutahiniwa.

2 comments

Leave a reply

Start a conversation.
Hi! Click on one of our members below to chat on WhatsApp.
The team typically replies in minutes.