Masomo katika nyakati za muunganisho wa kimtandao

0
683

Tofauti na Masomo ya nyakati za kale kabla ya uvumbuzi na matumizi ya mtandao, wanafunzi wa sasa wanayo manufaa chungu nzima. Ni vizuri kukumbuka kwamba wakati wa kale, wanafunzi walifaidi kwa mafunzo ya darasani kupitia kwa walimu na masomo ya ziada kutoka kwa vitabu walivyo vipata kwa maktaba. Tatizo kubwa lilikua uhaba wa vitabu na mkufunzi haswa kwa Masomo ya ziada. Vilevile, wanafunzi na walimu wakati huo walitumia muda mrefu kuchambua vitabu ama nakala zingine kupata somo lolote walilolitaka.

Baada ya uvumbuzi na muunganisho wa kimtandao, wanafunzi, walimu na wazazi wamepata sababu kubwa ya kutabasamu. Matatizo yaliyowapata wanafunzi na walimu katika nyakati za kale haswa kupata ujumbe maalum kupitia vitabu yameweza kupunguzwa kwa pakubwa. Wanafunzi wa nyakati za mtandao wanaweza kutumia mtandao kufikia ujumbe wa kimasomo kwa urahisi na kufaidika pakubwa kutokana na maandishi ya wataalamu wengi. Kwa njia ya kutafuta kupitia tovuti tofauti tofauti za kimtandao, wanafunzi wanafikia maarifa na kufaidika sana kimasomo.

Walimu vile vile wameweza kufaidika sana wakati wa mtandao ikilinganishwa na nyakati za kale. Kupitia kwa tovuti za kimasomo, jumbe nyingi za kimsingi za kurahisisha kazi ya kufunza na pia kuongeza maarifa kwao zinapatikana kwa urahisi kupitia kubonyeza tu ‘tafuta’ kwa vibonyezo vya kompyuta. Hivyo basi, kama vile wanafunzi wanafaidika kupitia kazi nyingi za kimasomo zilizoko katika mtandao, walimu pia wapata maarifa na hivyo basi kurahisishiwa kazi ya ukufunzi. Ni vizuri kufahamu kwamba jumbe za kimasomo zimetanda katika mtandao kutoka nchi tofatutitofauti na waandishi wengi hivyo basi kurahisisha masomo kwa njia kubwa.

Wazazi na wanaolinda watoto katika jamii pia wanayo manufaa tele kutokana na muunganisho wa kimtandao haswa kupitia mawaidha kutoka nyanja mbalimbali. Kupitia uchunguzi maalum, tovuti tofauti zinazo jumbe za manufaa sana kwa kuelimisha jinsi ya malezi, usalama kwenye mitandao na matumizi yanayofaa ya mitandao ya mawasiliano almaarufu social media kwa kingereza.

Mojawapo ya tovuti zinazowafaa sana wanafunzi, walimu na wazazi katika enzi zetu ni ‘Excellent Student Limited’ na ambayo imeundwa kiustaarabu na kwa umakini unaofaa kulinda haki za watumizi wote. Katika hii tovuti, utawezakupata jumbe za nasaha kupitia wataalamu tofauti tofauti haswa katika nyanja za teknolojia, masomo, mabadiliko ya dunia katika nyakati za mkurupuko wa virusi vya korona na mengineo. Wanafunzi na walimu wanafaidika pakubwa kupitia kazi za marudio, mitihani na majibu, na miongozo ya kimasomo iliyotayarishwa kwa ustadi sana na wakufunzi watajika kutoka shule za kitaifa nchini. Pia kipengee tofauti cha kazi mbalimbali za wanafunzi waliobombea katika nyanja tofauti kama utunzi wa shairi, insha, hadithi na tunzi zinginezo kimetengwa kusaidia kukuza vipaji. Hivyo basi, kila mtu anawezafaidika pakubwa kupitia tovuti yetu ya kimasomo.

Tembelea tovuti yetu na ambayo ni www.excellentstudent.co.ke  kupitia simu ya rununu ama tarakilishi na uweze kufaidika pakubwa na kuwa mbele kimasomo kupitia mtandao. Kumbuka kubonyeza ‘like’ na ‘subscribe’ ilimradi ufaidike kwa jumbe za ukumbusho tunapoweka nakala mpya za kazi zetu.

Leave a reply

Start a conversation.
Hi! Click on one of our members below to chat on WhatsApp.
The team typically replies in minutes.