Mtandao: Safina Ya Leo Kwa Biashara

0
569

Je wajua mtandao wawezakua wa manufaa kwa kila mfanya biashara?

Miaka michache iliyopita, wakati matumizi ya simu za rununu katika kijiji chetu yalionekana kutofautisha matajiri na walalahoi, ilikua nadra sana kumwona yeyote akibeba simu kama tunavyoona siku ya leo. Ikawa ndio sababu ndugu yangu alipofanikiwa kupata simu moja ya Erikson (Muundo wa kale uliokua na erio iliyotokezea), kila mwanakijiji angefahamu alipopita. Wakati ule, mawasiliano kupitia kupiga simu yakawa yanaonekana kama hali ya kitajiri. Miaka michache baadaye, mambo yakabadilika kiwango ya kwamba matumizi ya simu yalifanyika mambo ya dharura sana. Kadri muda ulivyosonga, ikafika wakati ambapo simu ya rununu isiyowezakuingia katita mtandao ilikosa maana haswa kwa vijana waliozaliwa baada ya 1980 almaarufu kizazi cha Y. Leo, matumizi ya kimtandao yamekua kiungo muhimu katika maisha ya kila mmoja kuanzia kwa matumizi ya kimsingi ya kirafiki hadi yale ya kibiashara na kiteknolojia.

Na ndiposa twajiuliza; je mtandao umekua kama safina ya leo?

Tunapowaza umuhimu wa mtandao katika maisha ya leo, tunatambua kwamba kila sekta imekua ya kuguzwa kwa njia moja ama nyingine. Baadhi ya sekta zinazohusika sana katika matumizi ya kimtandao ni biashara. Bila kutofautisha hadhi na kiwango cha Biashara, kila mwanabiashara anapata haja ya kuendeleza biashara yake kwa kuitangaza kupitia mtandao. Kwa wafanyabiashara wengine, matumizi ya kimtandao yanaenda zaidi ya matangazo na kufikia mauzo halisi kupitia hii teknolojia. Hivyo basi, imefikia nafasi ya kujiuliza swali lile la kimsingi; Je katika majira tunayoishi, mfanyabiashara awezakupuuza mtandao na akafaulu? Na je, mtandao una manufaa gani na hatari gani kwa bishara za leo?

Cha muhimu kulelewa katika muktadha huu ni kwamba kufaulu katika matumizi ya mtandao kwa biashara inategemea juhundi tofauti tofauti, haswa zinazohusiana na matangazo, miundo msingi ya kiteknolojia na hakikisho la usalama kwa watumizi na wateja. Jambo moja la kimsingi kila anayefikiria kufanya biashara kwa mtandao anapaswa kufahamu ni kuwa kuna hatari ya ukora unaohusisha mtandao. Watu wengi wanapofikiria kufanya ununuzi kupitia kwa njia ya kimtandao hupatwa na hofu ya kulaghaiwa na kupoteza mali yao. Wasomi wa matumizi ya mtandao wameonyesha faida kubwa zinazotokana na mauzo kupitia mtandao kwa biashara. Kati ya manufaa hayo ni pamoja na gharama iliyo chini ya matangazo, uwezekano wa kifikia watumizi wengi haraka na kwa njia ya urahisi ya kupokea maoni kutoka kwa wateja. Ila kuna haja ya kufahamu kwamba tishio la ulaghai wa kimitambo kupitia mtandao umeenea sana na unaezasababisha bishara ikaporomoka ama isifaulu. Hivyo basi, njia moja ya kuwezakufaulu katika biashara kupitia mtandao ni kuhakikishia watumizi na wanunuzi usalama wao.

Kunazo njia nyingi za kuhakikishia wanunuzi usalama wao kupitia mtandao ambazo ni pamoja na:

  • Linda data za kidigitari: Data ya watumizi wa mitandao ni ya umuhimu sana tunapoongea kuhusu usalama wa kimtandao. Kwa kawaida, kila mtumizi wa mtandao anapaswa kuacha taarifa muhimu za siri na ambazo walaghai wa kimtandao wanawezakutumia kumfikia na kumlaghai mteja. Hivyo basi, inapasa muuzaji yeyote atahadhari anavyotumia na kulinda zile taarifa kwa maana kwa njia ile, wanawezakushinda imani ya mnunuzi.
  • Hakikisha biashara haikusanyi takwimu zisizohitajika: Ina haja sana kwa kila anaetumia mtandao kufanya biashara kuhakikisha kwa taarifa anazokusanya za wateja ni zile tu zinahusika na mauzo yanayojarajiwa. Hii ina manufaa ya kwamba katika ule mtandao, watumizi wasio halalishwa hawafikii jumbe zingine zinazohatarisha usalama wa watumizi.
  • Punguza uwezekano wa watu wasiohalalishwa kufikia data za wateja: Yafaa sana kuwa katika hali ya kuunda mtandao wa kibiashara, mtaalam ahakikishe kwamba njia zote ambazo watumizi wasiohalalishwa wanawezatumia kuingia dani zimezibwa. Haja ya hakikisho lile ni kuwa wanunuzi watakua salama wakati data za kibinafsi hazitumiki na wasiohalalishwa.
  • Kutotegemea njia moja pekee ya kiusalama: Wataalam wa kuunda mitandao wanazo njia mbadala za kuhakikisha muuzaji na wateja wako salama. Hivyo basi, kwa kutumia njia nyingi za kuhakikisha mtandao uko salama, mwenye biashara atapata faida ya kuaminika na wateja na hilo lisanufaisha biashara.
  • Hakikisha uimalishaji wa usalama kwa mtandao unafanywa mara kwa mara: Yawezekana kwamba teknolojia iliyotumiwa kuunda mtandao imepitwa na wakati hivyo basi kuhatarisha matumizi yake. Hivyo basi, inampasa mfanya biashara yeyote wa kimtandao kuhakikisha anaimalisha usalama mara kwa mara kuzidisha umakini katika jitihanda za kuwalinda wateja.

Cha muhimu sana kwa watumizi wa mitandao ni hakikisho la kua data zao hazipotei na kua ununuzi wao utafaulu bila ulaghai. Hivyo basi, inawapasa wafanya biashara wote kuwekeza katika mikakati ya kuhakikishia wanunuzi usalama wao. Bila uhakikisho, biashara yawezakupoteza mauzo mengi kupitia hofu ya wanunuzi. Pia, tofauti kati ya biashara zinazofaulu na zinazoanguka katika nyakati za matumizi ya mtandao yanaonekana haswa kupitia uwezo wa mwekezaji kuhakikishia wateja usalama wao. Ni kwa ajili ile ambapo mtandao wa Excellent Student Limited (excellentstudent.co.ke) umeundwa hususan kuwawezesha watumizi wa kimtandao kupata habari za kimsingi za matumizi ya mtandao yanayofaa na ambazo zitafaidi wafanya biashara na wateja watarajiwa. Waweza ukauliza swali lolote na dharura kuhusu usalama wa kimtandao kwa kupitia tovuti yetu na utasaidiwa ipasavyo.

Kwa wafanyabiashara na wanunuzi, mtandao utabaki safi, hali ambayo itatofautisha kati ya wanaofaulu na wengine. Kutoka ESL, tunawahimiza kutumia mtandao katika bishara kwa sababu hatuweziendelea kutumia njia za kale za kufanya biashara na tutarajie kufaulu katika enzi za teknolojia

Leave a reply

Start a conversation.
Hi! Click on one of our members below to chat on WhatsApp.
The team typically replies in minutes.